Lissu amefanikiwa kuubwaga tena upande Jamuhuri uliofungua kesi...

@fbuyobe
Fortunatus Buyobe@fbuyobe
14 views Aug 01, 2026 ~4 min read
Advertisement
1
Lissu amefanikiwa kuubwaga tena upande Jamuhuri uliofungua kesi mahakama ya rufaa kupinga maamuzi ya mahakama kuu katika kesi ya jinai inayomkabili Lissu.

Si vibaya tukipata “a quick refresher” katika kesi ile ya uhaini hadi kuelewa tumefika vipi hapa
Media image
2
Lissu alikamatiwa Mbinga akiwa kwenye mkutano wa hadhara kunadi sera ya Chadema ya No Reforms No Elections

Akasafirishwa mpaka Dar Es Salaam ambako alifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya uhaini.
Media image
3
Ilidaiwa kuwa, Lissu alinaswa na chombo cha habari cha JamboTv akisema kuwa “tutafanya uasi” na “kukinukisha”

Ili kuiokolea mahakama muda, Lissu alikili kuwa yale ni maneno aliyoyatamka kweli na kwa vyovyote vile hayazai kosa la uhaini.
Media image
4
Lissu alifanya hivi trickery, ili jamuhuri isijusumbue kuleta mashaidi wa kuizungumzia video iliyorekodiwa akitamka hayo na hivyo kuokoa muda wake wa utetezi.

Lissu alishajua kuwa Jamuhuri haina kesi bali inataka kuiba muda huku akisota mahabusu hivyo mbinu hii ilikuwa ni ya kupunguza muda wa utetezi mahakamani. Pia kuinyima Jamuhuri fursa ya “delay tactics”
Media image
5
Jamuhuri ikiwa haina karata yoyote ya kucheza mahakamani zaidi ya video ile, ikalazimisha “kimenomeno” kuwapeleka mashaidi wa siri ambao wote walikuwa wakiongelea swala la video iliyorekodiwa.

Lissu akawafanyia dissection ya kikatili mashaidi hawa “in their hairy tennis balls with a burdizzo”

Wataalamu wa mifugo wanaita hii process “castration”
Media image
6
Lissu aliwashukia kama tai mashaidi hawa waliokuwa ndani ya kizimba kinachoning’inia kama tundu la njiwa.

Ingawa hawakutaka kufahamika, wengi wao waliweza kufahamika kupitia madodoso hadi Lissu mwenyewe akawa anawacheka kwa dharau Jamuhuri akiwauliza ni nini walichoficha?
Media image
7
Kupitia masterpiece cross-examination alizowafanyia Lissu mashaidi hawa aliweza kuonyesha jinsi ushaidi hao walivyokuwa incompetent na inconsistent.

Demeanor ya mashaidi hawa ikakosa worthwhile credibility kwa mujibu ya sheria ya ushaidi.

Mwisho kabisa Lissu akafanikiwa ku“expunge” kielelezo cha video iliyorekodiwa.

Naam!

Kielelezo ambacho ndio ilikuwa roho ya prosecution case
Media image
8
Kukosekana kwa video hii kama kielelezo cha ushaidi kulikuwa kunaenda ku“deprive” the all prosecution’s witness in chief of corroboration of another independent evidence” (kukosa ushaidi mwingine wa kuunga mkono uhaini)

Haya yalikuwa yanaendelea huku tukielekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oct 29, 2025

Lissu akarudi Makwaya na sisi tukaendelea na kampeni hadi siku ya uchaguzi.
Media image
9
Kwenye uchaguzi ule “kikanuka”, nchi “ikanuka”

Siku Lissu alipofikishwa mahakamani akawa anatoa tabasamu kama lile la kusuta la “si niliwaambia?”

Hapo ndipo Jamuhuri ikapanda mahakamani na notice mpya.

Kuwa inataka kuongeza ushaidi na vielelezo vingine vya ziada kupitia shaidi aliyekwishatoa ushaidi mahakamani (ACP Amini Kahamba)
Media image
10
Lissu akapinga utaratibu huo kwani sheria inataka kila ushaidi unapaswa kuwekwa wazi wakati wa committal katika mahakama ya ukabidhi.

Kuwa kufanya hivyo kunakuwa kumekiuka haki yake ya kuwa amesomewa mashitaka yake yote na ushaidi utakaotumika dhidi yake ili awe na nafasi nzuri ya kujitetea.

Kuwa mashtaka huwa hayaji kwa mtindo wa kuvizia kama komborela.
Media image
11
Pia Lissu akahisi jamuhuri inataka kuongeza ushaidi ili kumpa kichwa cha Mo29 wakati alikuwa makwaya.

Hata hivyo baadae zikasambaa taarifa mtandaoni kuwa shaidi wa siri ACP Mahamba alishafariki siku nyingi, mkewe akiwa amempost kwenye mtandao wa facebook akiomboleza msiba wake.

Hapa watu wakabaki na kitendawili juu ya authenticity ya mashaidi wengine wake siri.
Media image
12
Mahakama ikakubaliana na mapingamizi ya Lissu dhidi ya kuongezwa ushaidi na vielelezo vya ziada.

Siku ya maamuzi haya, mawakili wa serikali walirudi mahakamani baada ya mapumziko ya mlo wa mchana wakiwa wamekata tamaa kabisa.
Media image
13
Ghafla mawakili wa jamuhuri wakaibuka na kusudio la kukatia rufaa maamuzi ya mahakama kuu wakitaka mahakama ya rufaa ipitie upya maamuzi ya mahakama kuu kukataa kupokea kielelezo cha video na kukataa kuongeza ushaidi.

Ndio leo mahakama ya rufani imepiga mweleka maombi hayo

Hii inamaanisha nini?
Media image
14
Hii ina maana kuwa, kama Jamuhuri imeweza hata kutaka kuongeza ushaidi na vielelezo vya ziada kupitia “marehemu” Mahamba, inamaana imeshamaliza kutoa ushaidi wake mahakamani

Kisheria inataka kila maana “prosecution case is closed”
Media image
15
Kama upande wa mashtaka umeshafunga ushaidi wa kesi yake ya uhaini, kilichobaki ni kwa majaji wa mahakama kuu kutizama ushaidi huo na kuu“gauge” kama ume“establish” a prima facie case?
Media image
16
Yaani kwa benefit of doubt ambayo mtuhumiwa Lissu amepewa kuwa huenda hajatenda uhaini (presumption of innocence), lakini kupitia ushaidi uliofikishwa mahakamani na Jamuhuri, majaji wameshawishika kumshuku, Lissu kuwa ana kesi ya kujibu?
Media image
17
Binafsi sioni kama kuna prima facie case, kwa vigezo wa kielelezo kikuu kilichopigwa chini.

Kesi imeshapooza kwa msiba wa shoga!

Kilichobaki ni kwa Jamuhuri kuchutama na kuweka mpira kwapani kupitia “Nolle Prosequi”

Yani DPP atoe notice ya kutotaka kuendelea kumshitaki Lissu.
Media image
18
Kwa upande wangu naona serikali inaweza kuidaka vizuri fursa hii kwa kumwachia Lissu ili kupata reconciliation na jumuiya ya kimataifa inayoibana hadi kutoa ultimatum ya mwezi mmoja kumaliza kesi ya Lissu.

Hii haitakuwa udhaifu kwa serikali bali utakuwa ni ukomavu ambao utaweza kutufungulia tena fursa za uchumi pamoja na mikopo nafuu

End of night rant hoofmen
Media image
Actions
What You Can Do
  • Export as PDF or Markdown
  • Batch Export to Notion
  • Bookmark & Highlight
  • LinkedIn & Instagram Carousel Maker
Create Free Account

Includes 7-day Premium trial

Advertisement